Hi karibuni meneja wa wasanii wa record label za Tiptop Conenction na WCB Wasafi ndugu Hamisi Taletale almaarufu kama Babu Tale alihojiwa na Team ya 255 ya Clouds FM kuhusu ni wasanii gani amekwisha fanya nao kazi na anatamani wangerudi tena kuwa chini ya uongozi wake.
Bila kuficha Babu Tale aliwataja Z. Anto, Kassim Mganga na Keisha kwamba ndio wasanii ambao huwa anawakumbuka hadi leo kwasababu walikuwa na vitu vya Tofauti wakati anafanya nao kazi.
Aliongeza kwa kusema yeye na Kassim Mganga walielewana sana kwa sababu Kassim alikuwa na tabia za uongo uongo na umbea ndio sababu zilizo wafanya waelewane sana kwasababu na yeye ni mtu mwenye tabia hizo, kwahiyo walikuwa wakitumia muda mwingi kwa kuteta.
Kwa upande wa Keisha alisema yeye ni rafiki yake tokea kitambo kwa sababu walisoma wote kipindi cha nyuma na hivyo kupelekea urafiki wao kunoga kwa sababu ni watu wanaofahamiana toka zamani.
Msikilize hapa Babu Tale akizungumza juu ya hilo.
Title :
(+AUDIO) NATAMANI Z. ANTO NA KASSIM MGANGA WANGERUDI TIP TOP-;BABU TALE
Description : Hi karibuni meneja wa wasanii wa record label za Tiptop Conenction na WCB Wasafi ndugu Hamisi Taletale almaarufu kama Babu Tale alihojiwa n...
Rating :
5