Young Dee ni msanii ambaye amekuwa na skendo nyingi ambazo zimekuwa zikimuhusisha yeye na utumiaji wa madawa ya kulevya lakini alikuwa akikanusha kuhusu swala hilo kila anapokutana na vyombo vya habari.
Jana June 22 Rapper huyo hit maker wa nnyimbo kamaKijukuu, Siyo mchoyo na nyingine kibaao aliitisha mkutano na vyombo vya habari kuweza kulizungumzia swala hilo na kukiri kuwa ni kweli yeye kama kijana alipitia maisha ya utumiaji wa dawa za kulevya ila kwa sasa ameacha.
Mkutano huo ulikuwa ukihusisha pia jambo la yeye kurudi rasmi katika uongozi wake wa zamani ambao walitofautiana miezi kadhaa iliyopita.
"
Hakuna mtu yeyote ambaye naweza kumlaumu tofauti na mimi mwenyewe kutokana na mazingira ambayo nimekuwa nikipitia, unajua watu wengi hawafahamu mimi nimetoka wapi au nimelelewa vipi malezi yangu kifamilia yalikuwa vipi. Nimepitia maisha ambayo sikuwa na watu ambao wanaweza kuniona nafanya kitu kibaya wakanichekea yani nimepitia maisha flani ya makundi.
Ningepennda kutoa ushauri kwa vijana wenzangu wawe waangalifu kwa vijana ambao wanawazunguka, kwa sababu katika maisha ukitembea na wezi wawili basi tegemea kuwa mwizi wa tatu. Juhudi zangu ndo zimenifikisha hapa kunisaidia kuachana na mambo yale kwa sababu kuichagua hii familia ni kuwa najua sintokuwa tena na watu ambao wanaweza kunishauri chochote kuhusu kule tena" Alisema Young Dee.
UNGANA NASI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KAMA
INSTAGRAM
FACEBOOK na TUTUMIE EMAIL KWA HABARI AU JAMBO LOLOTE
Title :
NI KWELI NIMETUMIA MADAWA (DRUGS) LAKINI SIKUWA MUATHIRIKA -; YOUNG DEE
Description : Young Dee ni msanii ambaye amekuwa na skendo nyingi ambazo zimekuwa zikimuhusisha yeye na utumiaji wa madawa ya kulevya lakini alikuwa akika...
Rating :
5