Kama ni mpenzi wa muziki wa bongo fleva wakizamani kidogo basi huwezi kuwa hulijui kundi la muziki lililo fanya vizuri sana miaka ya Elfu mbili la TMK WANAUME. Ambalo lilikuwa likiundwa na vichwa kama Juma Nature, KR Mula, Chege Temba na wengineo kibaao.
Kundi hilo lilivunjika kwa matofautiano ya kimaslahi na kupelekea kuundwa kwa makundi mawili ambayo ni TMK WANNAUME FAMILY na TMK WANAUME HALISI ambpo Halisi iliundwa na Juma Nature na wafuasi wake na FAMILY iliundwa na wasanii kama Chege na Temba ambao ndio walio bakia katika uongozi wa mwanzo kabla ya kun ndi hilo kuvunjika (Uongozi wa Saidi Fela).
Mvunjiko huo ulipelekea baadhi ya wasanii kukata tamaa kimuziki kwa kudhani kuwa muungano ule ndio ulikuwa nguzo kwao lakini ilikuwa tofauti kwa wasanii kama Chege ambao walibaki chini ya uongozi wa Saidi Fela ambao waliendelea kutoa vibao kama Kazi ipo na Dar mpaka Moro na zikaendelea kufanya vizuri na kuweza kuwapa moyo kwamba wanaweza kusonga mbele bila muungano ule.
Wapo wapenda muziki ambao walikuwa wakipendezwa na muungano ule mmoja wao ni raisi wa awamu ya nne wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye kwanamna moja ama nyingine alikuwa akivutiwa na muziki wanaoufanya kama kundi kwa pamoja na akaona kuna vitu vimekosekana baada ya mvunjiko ule wa kundi na kuchukua jukumu la kuwaita wasanii kama Chege na kuwauliza nini tatizo na kuwataka warudi katika muungano na kuendelea kufanya muziki kama zamani.
"President alitwita kabisa ikulu kutaka kutuweka pamoja kundi lisije likavunjika kwasababu point yake ya msingi alikuwa anasema kwamba akizunguka mikoani hadi mashuleni kwenye dawati za wanafunzi anakuta zimechorwa (zimeandikwa ) TMK WANAUME FAMILY. na kutuuliza kwamba ni kwanini tunaua brand ambayo ni kubwa kabisa!? Lakini haikuwezekana kwasababu wachache tulifika wengine hawakufika." Alisema Chege.
Title :
TULIWAHI KUITWA NA RAISI KUTAKA KUIRUDISHA TMK WANAUME -; CHEGE
Description : Kama ni mpenzi wa muziki wa bongo fleva wakizamani kidogo basi huwezi kuwa hulijui kundi la muziki lililo fanya vizuri sana miaka ya Elfu ...
Rating :
5