Tajiri wa mahaba toka manzabey Tanga Kassim Mganga amezungumza kuwa hawezi tena kurudi katika uongozi wake wa zamani TIPTOP CONNECTION.
Amezungumza hayo alipo hojiwa na Asteria Mvungi wa TZA studios za Millard Ayo.
"Ile ni familia yangu, ikitokea tufanye kazi tunafanya lakini si kwa kurudi moja kwa moja pale. Kwasababu bado nifamilia, bado tunawasiliana vizuri tu bado tupo pamoja kwenye shida na raha tunakimbiliana kwahiyo kuna uwezekano wa kuweza kufanya lolote ikiwa Manzabay Company na Kampuni yangu ya Dar Staminah tume join na Tiptop Connection linaweza likatokea jambo. Alisema Kassim mganga.
Kassim mganga ni msanii ambaye amekaa chini ya Tiptop Connection kwa zaidi ya miaka mitano na wiki moja iliyopita meneja wa Tiptop Connection alisikika akisema kuwa kama kuna wasanii anatamani warudi afanye nao kazi na jina la Kassim Mganga lilisikika kati ya aliowataja.
Inaonyesha ni jinsi gani wawili hao walikuwa vizuri na walifanya kazi kwa ushirikiano na uelewano wa hali ya juu.
UNGANA NASI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KAMA
INSTAGRAM
FACEBOOK na TUTUMIE EMAIL KWA HABARI AU JAMBO LOLOTE
Title :
SIWEZI KURUDI KUJIUNGA TENA NA TIP TOP CONNECTION -; KASSIM MGANGA
Description : Tajiri wa mahaba toka manzabey Tanga Kassim Mganga amezungumza kuwa hawezi tena kurudi katika uongozi wake wa zamani TIPTOP CONNECTION. A...
Rating :
5