Raymond (Rayvanny) ni msanii mwenye kipaji na uwezo wa hali ya juu katika tasnia hii ya muziki nchini Tanzania, anatoka chini ya label ya WCB, Raymond ana uwezo mkubwa katika uandishi wa mashairi na kutengeneza melidy za muziki.
Raymond amesha shiriki katika utengenezaji wa ngoma nyingi na kali na zikafanya vizuri, baadhi ya ya ngoma hizo ni pamoja na Shikorobo ya Sheta, Zigo remix ya AY aliyomshirikisha Diamond Platnumz ambae ni Bosi wa Raymond, katika ngoma hiyo raymond alishiriki kwa kuongeza melodies baadhi ambazo zilikuwa ziki mtatiza Bosi wake Diamond Platnumz.
Zingine ambazo zimepita katika mikono ya Raymond ni kama Sio mchoyo ya Young Dee, Make me Sing ya A.K.A na Diamond na nyinginezo kibaao.
Msikilize hapa mwenyewe Raymond mwenyewe akizungumzia juu ya uwezo wake huo.
Title :
ZIFAHAMU HIT SONG AMBAZO ZIMEPITA MIKONONI MWA RAYMOND WA WCB
Description : Raymond (Rayvanny) ni msanii mwenye kipaji na uwezo wa hali ya juu katika tasnia hii ya muziki nchini Tanzania, anatoka chini ya label ya WC...
Rating :
5