Ben Pol nni msanii mkongwe katika muziki huu wa bongo fleva na alie jizolea sifa kibao katika aina ya muziki anaoufanya na kupachikwa jina la King of RnB, yote hiyo ni kutokana na kufanya kwake vizuri katika kazi yake anayoifanya.
Ben Pol ameshatengeneza Hit kibao kama Nikikupata, Samboira,Maneno manenno nna nyingine kibaao tukiachilia mbali hii inayofanya vizuri kwa sasa inayoitwa Moyo Mashine.
Ben anaamini ili msanii ukamilike na uwe na sifa zilizo kamilika kama msanii ni lazima uwe na albam, Ben Pol amefanikiwa kutengeneza albam mbili na hii anayotaka kuiachia sasa hivi ita kuwa ni ya 3 ambayo amesema ataiita MALI YA BEN POL.
"Hivi natengeneza album nyingine ya tatu ambayo itaitwa Mali (Mali ya Ben Pol), ambayo hiyo albam mwenyezi mungu akijalia inatoka muda sio mrefu, labda ndani ya mwezi mmoja au miezi miwili kwasababu nipo kwenye hatua za mwisho, na nimeirekodi kwa mwaka na nusu hiyo albam" Alisema Ben Pol.
Title :
BEN POL NA MIPANGO YAKE YA KUTOA ALBAM
Description : Ben Pol nni msanii mkongwe katika muziki huu wa bongo fleva na alie jizolea sifa kibao katika aina ya muziki anaoufanya na kupachikwa jina...
Rating :
5