Kama ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii na Baraza la wawakilishi Yanzania (Bunge) najua jina la Godluck Mlinga litakuwa si geni katika maskio yako.
Kama bado huja sanuka ni <bunge ambaye May 13 mwaka huu alisimama bungeni na kusema kuwa
"Ingekuwa amri yangu tungechonga sanamu la Diamond Platnumz na tukaliweka kwenye mnara wa askari ule mnara tumeuchoka, Diamond ametufikisha mbali na ameitangaza nchi yetu huko mbele"
Nadhani umepata picha nini namaanisha, sasa achana na Godluck Mlinga, leo kipaza cha 255 kimesogezwa mkongwe wa muziki wa Hiphop Tanzania ndugu Suleiman Msindi (Afande Sele ) na kuulizwa analizungumzia vipi suala hili la mbunge kuzungumza maneno yale katika bunge tukufu. Na haya ndio yalikuwa majibu yake
"Sikutegemea mtu wa aina ile anaweza kwenda kuongea jambo la namna ile katika bunge tukufu, anafikia hadi hatua ya kulidhalilisha jeshi la polisi, Jeshi ndio linalinda nchi yetu, kuna wanajeshi wamekufa hawana idadi kwa sababu ya kupigania nchi yetu, sasa leo anakuja mbunge, ubunge wenyewe ameupata kama mtu ana kabidhiwa chupa ya chai, yani mtu anapata ubunge kwa sababu tu mama yake alikuwa mbunge, na uzuri wa nchi yetu ujinga umetamalaki, watu wanampa kura matokeo yake anakua hana cha kuzungumza akiwa katika bunge tukufu. Mwisho wa siku analidhalilisha Jeshi kwa kusema mwanajeshi aliyepigania nchi atolewe na awekwe Diamond kwakuwa tu anaimba! kweli Diamond anafanya kazi nzuri, ni mwana muziki lakini huwezi kusema yeye ni mwanamuziki zaidi ya Mr Nice,Mr Nice ndio msanii alio andaa muziki wake wa TAKEU muziki ambao hauja imbwa na msanii yeyote kabla, labda yeye ndio angestahili sifa hiyo! Kwa maoni yangu Jeshi ilitakiwa imchukulie hatua haraka sana. Mimi nigekuwa Jeshini na ningepewa cheo kipindi hiki yule Mbunge siku nyingi ningekua nimesha mkata ngwala nyingi, Kwasababu huwezi kumtoa mwanajeshi kamanda aliye mwaga damu kwa sababu ya nchi hii na ukamuweka mtu ambaye anaimba tu! kibaya zaidi muziki wenyewe ume base kwenye viuno."
Kama ulikuwa hujajua Afande Sele ni mwanajeshi mwenye sifa zote hata kama leo hii ikitokea vita mwana Hiphop huyo atajumuika kwenye hilo.
Title :
NINGEKUWA NA CHEO JESHINI! NINGESHA MCHEZESHEA VITASA MBUNGE ALOSEMA LITOLEWE SANAMU LA ASKARI LIWEKWE LA DIAMOND -: AFANDE SELE
Description : Kama ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii na Baraza la wawakilishi Yanzania (Bunge) najua jina la Godluck Mlinga litakuwa si geni katika ...
Rating :
5