Rhymes Of Magic Attraction hiyo ni definition ya jina la msanii anayefanya muziki wa Hiphop Tanzania
ROMA ambaye jana ameachia rasmi nyimbo yake mpya ambayo ameipa jina la "Kaa Tayari"
Kwenye nyimbo hiyo amewashirikisha wasanii wenzake ambao pia wanafanya muziki wa Hiphop Darasa na Jos Mtambo.
Kwenye nyimbo hiyo kuna mstari ambao
ROMA amelitaja jina la meneja wa
Diamond Platnumz na Tiptop Connection (Babu Tale) ambavyo imechukuliwa kama diss kwa meneja huyo kutokana na jinsi
ROMA alivyo mzungumzia katika mstari huo.
"Bosi kamganda Dangote kaisahau Tiptop" ni mstari ambao ameuimba
ROMA akimuhusisha meneja huyo wa
Diamond Platnumz (Chibu Dangote) na Tiptop Connection katika nyimbo yake hiyo mpya.
Babu Tale amekuwa na lakuzungumza baada ya kuvutiwa waya (Kupigiwa simu) na Perfect255 na kuulizwa juu ya jambo hilo na aliyo yazungumza ni haya hapa chini.
"Roma ni mtu ambaye huwa anaandika mashairi baada ya kusikiliza habari katika radio au televisheni, sasa vitu anavyo vifanya raisi John Magufuli kwa sasa ni vitu ambavyo ROMA hawezi kuviandika kwahiyo inambidi aje kwa watu kama sisi, Ni kawaida! Kwahiyo usipo msapoti ROMA utakuwa humtakii maisha mema kwenye muziki, utakuwa unatamani ROMA apotee, kitu ambacho sio kitu kizuri utapata dhambi, Kwahiyo sasa hivi anahamia huku sasa (kwenye ku diss) wakati huku siyo kwake huku ni kwa Nay wa Mitego" Alisema Babu Tale.
Na pia akaongeza kuwa uchapakazi wa Raisi Magufuli unaweza kumpelekea
ROMA asjindwe kuandika nyimbo kwa sababu
ROMA alikuwa anasubiri taarifa ya habari itoke ndio aandike nyimbo. "Akifanya masihara kwa jinsi Magufuli anavyo endelea kufanya kazi kwa nguvu ataua kipaji" Alimaliza kwa kusema hivyo meneja huyo wa
Diamond Platnumz na Tiptop Connection Babu Tale.
Ungana nasi katika mitandaoyakijamii kama
INSTAGRAM
FACEBOOK na tutumie
EMAIL kwa taarifa aujambo lingine lolote.
Title :
Alicho kisema Babu Tale baada ya Roma kum-dis kwenye nyimbo yake mpya ya "Kaa Tayari"
Description : Rhymes Of Magic Attraction hiyo ni definition ya jina la msanii anayefanya muziki wa Hiphop Tanzania ROMA ambaye jana ameachia rasmi nyim...
Rating :
5