Usiku wa kuamkia leo yani usiku wa July 14 majira ya saa 3-4 usiki msanii Diamond Platnumz alitoa muda wa lisaa lizima (1) kwa mashabiki zake kuweza ku chat nayeye live na kumuuliza maswali yote ambayo wanajisikia kumuuliza nayeye kuwajibu papo hapo katika mtandao wa Instagram.
Ni zaidi ya Comments 3800 zilipatikana ndani ya muda huo kutoka kwa mashabiki wa msanii huyo kumuuliza maswali mengi na wachache walifanikiwa kujibiwa maswali yao.
Moja kati ya maswali aliyo ulizwa Diamond Platnumz ni pamoja na
"Bro unafikiri muziki wako utachukua miaka mingapi ili ku hit marekani kama unavyo kick sasa Afrika!?" swali ambalo aliulizwa na shabiki wake anayetumia jina la @godfreymateru14 katika mtandao huo wa Instagram na Diamond Platnumz akamjibu
"Inshaallah nipe miezi 12"
Swali lingine alilo ulizwa ni kwamba
"Ni process gani ambazo msanii mchanga anatakiwa kuzitumia ili kuweza kafanya kazi na wasanii ambao anawasimamia yeye katika lebo yake ya WCB!? Wasanii kama Raymond, Harmonize na Rich Mavoko!"
"Awe mkali na awe na uwezo wa kushoot video bora na promo ya ngoma" Na hilo ndilo lilikuwa jibu la Diamond Platnumz kwa @romeoplatnumz_ ambaye ndiye alio muuliza swali hilo.
Ni kitu kizuri na kinafaa kuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine kuwa wanatoa muda wa kuzungumza na mashabiki zao kwasababu inasaidia kwa msanii kujua kilichomo katika fikra za mashabiki zake na kujua nini wana hitaji kwa wakati huo.
Title :
Nina miezu 12 tu ya kutusua nje ya Afrika -: Diamond Platnumz
Description : Usiku wa kuamkia leo yani usiku wa July 14 majira ya saa 3-4 usiki msanii Diamond Platnumz alitoa muda wa lisaa lizima (1) kwa mashabiki z...
Rating :
5