Msanii kutoka WCB Wasafi hit maker wa single ya Bado nyimbo ambayo amemshirikisha bosi wake Diamond Platnumz, Harmonize amefunguka ya moyoni juu ya hisia zake kuwa anatamani sana kufanya kazi na msanii nguli wa Bongo Fleva Dully Sykes.
Akihojiwa katika kipindi cha OnPoint kinacho ruka Clouds FM kila Jumapili saa 10 hadi 12 Jioni na Perfect Crispin aliongea hayo baada ya kuhojiwa kuwa ni msanii gani anatamani kufanya nae kazi kwa sasa nchini, Na haya ndio yalikuwa majibu yake
"Dully Sykes, me napenda the way anavyoimba halafu ni wa siku nyingi lakini bado anaonekana ana shine, kwanza bado ana muonekano kama ni msanii wa mwaka jana, kitu kingine napenda the way anaimba, napenda style pia napenda anavyo weza ku maintain mpaka leo bado yupo kwenye game! I WISH SIKU MOJA NIFANYE NAE KOLABO"
Harmonize alizungumza pia ni vitu gani ambavyo anatakiwa kufanya mtu ambaye anahitaji kufanya kazi na yeye
"Ukitaka kufanya kolabo na mimi we andaa nyimbo nzuri tu, hicho ndio kitu cha msingi kwasababu tukifanya ngoma ikiwa hit hata mimi pia itanitengenezea mazingira mtaani kuwa Harmonize kafanya kolabo na ime hit, sio tufanye kolabo" Alisema Harmonize
Harmonizee alikwenda kuitambulisha Audio ya nyimbo yake mpya inayoitwa Matatizo. Nyimbo ambayo inafanya vizuri kwa sasa mtaani kiasi kwamba video yake imefikisha viewers zaidi ya Millioni moja (1,000,000) katika Youtube ikiwa ina wiki moja tu tangu ameiachia.
Title :
NATAMANI KUFANYA KAZI NA DULLY SYKES -: HARMONIZE
Description : Msanii kutoka WCB Wasafi hit maker wa single ya Bado nyimbo ambayo amemshirikisha bosi wake Diamond Platnumz, Harmonize amefunguka ya moyo...
Rating :
5